Diarra awashusha presha mashabiki, Aitabiria ushindi Yanga

Diarra awashusha presha mashabiki, Aitabiria ushindi Yanga

Kikosi cha ‘klabu’ ya #Yanga kimerejea jijini Dar es Salaam alfajiri ya jana na moja kwa moja kwenda kambini kujiandaa na ‘mechi’ ijayo ya Kundi D ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Al Ahly ya Misri, huku ‘kipa’ tegemeo wa ‘timu’ hiyo, Diarra Djigui akiwatuliza mashabiki akiwataka waondoe hofu.

Kipa huyo raia wa Mali alifunguka juu ya hali yake kwa kushindwa kudaka ‘mechi’ hiyo ya kwanza, lakini akiwatoa hofu mashabiki na kuwataka kujitokeza kwa wingi kwenye mchezo ujao utakaopigwa kwa Mkapa.

Akizungumza na Mwanaspoti, Diarra amesema “Naendelea vizuri na ninafanya mazoezi na wenzangu, tatizo langu la bega halikuwa kubwa ila lilihitaji kupata mapumziko ya muda mrefu kiasi ili kujiweka hali nzuri ya ushindani nafikiri muda ukifika mtaniona uwanjani,” amesema Diarra na kuiongeza,

“Siwezi kuweka wazi ni lini ila nipo kwenye hali nzuri mashabiki watarajie kuniona uwanjani muda wowote nafurahia upendo wao kwangu, nimepokea ‘meseji’ nyingi kutoka kwa Wanayanga na ninawahakikishia hatutawaangusha.”

Kuhusu mechi iliyopita, Diarra amesema “Tumepoteza, hii ni sehemu ya matokeo tumeumia, ila tunajipanga kwa mchezo mwingine ambao ni muhimu zaidi dhidi ya Al Ahly nyumbani hatuwezi kurudia makosa tunahitaji point zote tatu ili kurudi kwenye mstari na mashabiki wajiandae kupata ile burudani waliyoizoea,” amesema kipa bora huyo wa Ligi Kuu Bara kwa misimu miwili mfululizo.

Cc.Mwanaspoti
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags