Diamond mbioni kudondosha  kolabo nyingine

Diamond mbioni kudondosha kolabo nyingine

Baada ya kutamba katika remix ya ‘Komasava’ aliyomshirikisha msanii wa Marekani Jason Derulo na kupokelewa kwa ukubwa, sasa mwanamuziki Diamond ameripotiwa kufanya ‘kolabo’ na staa wa muziki kutoka Morocco aitwaye Saad Lamjarred.

Ujio wa ‘kolabo’ hiyo umethibitisha na kampuni ya Diamond Wasafi kwa kuchapisha picha ya mkali huyo wa ‘Komasava’ akiwa studio na Saad ikiambatanishwa na ujumbe unaoeleza kuwa wawili hao wanatarajia kutoa ngoma hivi karibuni.

Utakukumbuka kuwa mwanamuziki huyo kutoka Morocco mwaka jana alitamba na wimbo wake wa ‘Guli Mata’ aliyomshirikisha staa wa India aitwaye Shreya Ghoshal ambao mpaka kufikia sasa una zaidi ya watazamaji milioni 370 katika mtandao wa YouTube.

Endapo ‘kolabo’ hii itafanikiwa kutoka basi Diamond atakuwa msanii wa kwanza kutoka Tanzania kufanya ngoma na staa huyo ambaye ni msanii wa pili barani Africa kuwa na wafuasi wengi katika mtandao wa Youtube ambao ni zaidi ya 15.3 milioni huku nafasi ya kwanza ikishikwa na msanii wa Misri Mohamed Ramadan mwenye Subscribers 15.6.

Diamond kwa sasa anatamba na video ya ngoma ya ‘Komasava Remix’ yenye zaidi ya watazamaji milioni 4 kupitia mtandao wa YouTube ikiwa na siku nne tuu tangu kuachiwa kwake.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags