Diamond kulipa  kodi 1.7 bilioni kwa mwaka

Diamond kulipa kodi 1.7 bilioni kwa mwaka

Unaambiwa bwana Staa wa muziki Tanzania na Africa kwa ujumla Diamond Platnumz ameweka bayana  kiasi cha kodi anacholipa kwa mwaka ambapo ni Tsh Bilioni 1.7. 

Diamond ameeleza hilo kwenye mkutano wa zoom ambao umekutanisha wadau wa siasa na viongozi mbali mbali kuelekea miaka 60 ya uhuru.

“Serikali imetengeneza mazingira rafiki kurasimisha tasnia ya muziki na kuiwekea wepesi kwenda kwenye sekta rasmi mfano mimi kutoka kwenye uwanamuziki mpaka nimekuwa mkurugenzi wa makampuni mbalimbali”

“Nilikuwa nafanya mahesabu hapa namna ya kimapato  huu mwaka kwa kodi ambazo tumezichangia ni bilioni 1.7, najivunia serikali imeniwekea mifumo sahihi najiona ni mlipa kodi na nachangia kwa namna moja au nyingine”alisema Diamond.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Saphinia Suleiman

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, career, skills development and technology.


Latest Post

Latest Tags