Diamond: Hilo busu lisiwatishe

Diamond: Hilo busu lisiwatishe

Uuuuwiiiiih! Nikiwaambia mapenzi yametaradadi kwa wasanii wetu wa bongo basi muwe mnanielewa, basi bwana kumekuwa na gumzo kupitia mitandao ya kijamii baada ya msanii anayetamba na kibao chake cha kwikwi, Zuchu kupigana mabusu na bosi wake njenje.

Diamond kupitia ukurasa wake wa Instagram alishare video ambayo alikuwa akipewa zawadi ya cheni kutoka kwa msanii wake Zuchu ambae anahusishwa kutoka nae kimapenzi kwa muda mrefu, ndani ya clip hiyo wawili hao walionekana wakipigana mabusu.

Kama kawaida yetu waja hatuishiwi na chakusema meneja wa msanii Diamond, Babu Tale amekomenti katika video aliopost msanii wake na kusema kuwa, “fanya uoe unanichelewesha ujue.” 

Basi bwana Cibudi Chibude hakuipuuzia ile komenti, aliijibu kwa kueleza kuw,a “Asa nitamuoaje wakati ni msanii wangu. Boss Hilo Busu lisiwatishe viongozi.Hhizo ni salamu za Kijerumani.''






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags