Diamond awaburuza Davido, Asake na Burna Boy

Diamond awaburuza Davido, Asake na Burna Boy

Nyota wa muziki wa Bongo Fleva Diamondplatnumz amekuwa msanii wa kwanza Afrika mwenye ngozi nyeusi kufikisha wafuasi milioni 8.66 kapitia mtandao wa YouTube.

Mafanikio hayo yanapelekea Diamond kuwaburuza wasanii mbalimbali wenye ngozi nyeusi wa Afrika akiwemo Burna Boy, Davido na Wizkid.

Msanii anayefuata baada ya Diamond kuwa na wafuasi wengi ni Burna Boy akiwa na 4.65 milioni, akifuatia Davido 3.88 milioni, Wizkid 2.99 milioni na Asake akiwa na wafuasi 1.09 milioni.

Aidha katika orodha iliyotolewa na tovuti ya ‘Pan African’ imeonesha kuwa mwanamuziki Diamond ni msanii wa tano kuwa na wafuasi wengi kwa Afrika nzima. Huku namba moja ikishikwa na Muigizaji na mwanamuziki wa Misri Mohamed Ramadan mwenye asili ya Kiarabu ambaye anaupiga mwingi kwenye nyimbo za Kiarabu akiwa na wafuasi 15.4 milioni.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags