Diamond anunua ndege binafsi ili kuonekana wa thamani

Diamond anunua ndege binafsi ili kuonekana wa thamani

Diamond Platnumz ni kati ya wasanii waliojizolea umaarufu sana Afrika na dunia kwa ujumla. Kutoka katika maisha ya hali ya chini sana, msanii huyu amefanikiwa kupanda kwa kiasi cha juu na kuwa kati ya wasanii bora Afrika, huku akishika namba moja kwa wasanii wa Afrika Mashariki.

Mafanikio hayo yamekuja pamoja na vitu vingi sana na msanii huyo hayawahi acha ku'brag' kuhusu vitu anavyomiliki, ikiwa pamoja na gari la kifahari, lenye thamani ya Bilioni 2.3.



Hivi karibuni katika interview yake na DW Africa nchini Germany, msanii huyu amedai kuwa amenunua ndege binafsi 'jet' ikiwa ni moja kati ya njia yake ya 'kujiheshimisha.'


 "Tayari Nimeshanunua Ndege," Diamond alisema alipokuwa akizungumzia namna msanii anatakiwa kuishi ili apewe heshima anayostahili na kuingiza mkwanja wa kutosha. 



Msanii huyo aliongeza kuwa, "Mfano kwa mtu kama mimi ambaye nimetokea mtaani, kwasasa nanunua gari la kifahari lenye thamani hadi bilioni 2.3/=...Kwahiyo itabidi ufanye hivyo kwani usipofanya hivyo hawatakuona wewe ni wa thamani ..na sasa tayari nimeshanunua ndege binafsi."

Haya sasa... unalionaje hilo? Je ni sahihi kununua ndege kwaajili ya kuwepa heshima tu? Tupia Comment yako.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Detricia Pamba

A Digital Journalist, Content Creation Executive at Mwananchi Communications Ltd and Chief Editor of Mwananchi Scoop. I'm also writes stories around Technology, every Wednesday on Mwananchi Scoop. My other famous segments on Mwananchi Scoop include LISTI and WHO’S HOT.


Latest Post

Latest Tags