Diamond, Alikiba kutoana jasho tuzo za TMA

Diamond, Alikiba kutoana jasho tuzo za TMA

Kamati ya uandaaji wa Tuzo za Muziki nchini (TMA) leo Agosti 29 imetangaza majina ya wasanii watakaowania tuzo hizo katika vipengele vitatu ambavyo ni Mwanamuziki Bora wa Kiume wa Mwaka, Wimbo Bora wa Taarabu wa Mwaka na Wimbo Bora Afrika Mashariki, Kusini na Magharibi.

Ambapo katika majina ya wasanii wanaowania kipengele cha Mwanamuziki Bora wa Kiume wa Mwaka lipo la Marioo wimbo wa ‘Shisha’, Diamond ‘Shu’, Harmonize ‘Single Again’, AliKiba ‘Sumu’ na mwisho ni Jay Melody na wimbo wa ‘Nitasema’.

Akizungumza na waandishi wa habari Makamu Mwenyekiti wa Tuzo hizo Christine Mosha ‘Seven’ ameeleza kuwa wameamua kutangaza vipengele vitatu ili kuwafanya mashabiki waendelea kufuatilia mchakato wa ugawaji wa tuzo hizo.

“Tumeamua kutoa kategori hizo tatu kwa ajili ya kuleta utofauti ambao utaleta impact ya tuzo kuongelewa kama tunavyoelewa kwenye eneo ambalo watu wanakuwaga na hamasa sana ya kujua mambo ya tuzo ni wakati wa nominees zinapotolewa, kwa hiyo tumeamua kubakisha tuu ili kuleta 'attention' kwa watu na mashabiki,” amesema Seven.

Upande wa Wimbo Bora wa Taarabu wa mwaka wanaowania ni pamoja na Malkia Layla Rashid ‘Watu na Viatu’,  Amina Kidevu ‘Hatuachani’ , Mwinyi Mkuu ‘Bila Yeye Sijiwezi’,  Mwasiti Mbwana ‘Sina Wema’ na Salha ‘DSM Sweetheart’.

Katika kipengele cha Wimbo bora Afrika Mashariki, Kusini na Magharibi yupo Libianca na ngoma yake ya ‘People’, Qing Madi ‘American Love’, Asake ‘Lonely at the Top’, Davido ft Musa Keys ‘Unavailable’ na Tyler ICU wimbo wa ‘Mnike’.

Kamati hiyo ya tuzo imeeleza kuwa vipengele vingine vitaendelea kutangazwa kila baada ya muda huku zoezi la kupigia kura likifumguliwa rasmi Septemba 3, 2024.

Ikumbukwe kuwa Tuzo za Muziki Tanzania zilianza kutolewa mwaka 1999 - 2014 mfululizo (miaka 16), kwa udhamini mbalimbali mwaka huo zikiwa zinaitwa Serengeti promotion - mwaka 1999, The Look Company - mwaka 2000 (Ziliitwa Dar es Salaam Awards) kwa miaka hiyo yote miwili.

Hata hivyo, ziliendelea kutolewa na TBL Ltd kwa mwaka 2003 – 2014, baadaye zilisimamishwa baada ya mabidiliko ya mfumo wa TBL Ltd lakini Baraza la Sanaa Taifa 'BASATA' lilifanikiwa kurejesha tuzo hizo zikiwa na jina la Tanzania Music Awards TMA mwaka 2021, kisha 2022 na sasa 2023 ambapo zinakuwa tuzo za 19 kutolewa Tanzania.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags