Diamond alia na serikali ukosefu wa Arena Tanzania

Diamond alia na serikali ukosefu wa Arena Tanzania

Mwanamuziki Diamond Platnumz ameiomba Serikali kutengeneza Arena kwa ajili ya matamasha makubwa ya muziki kama Trace.

Diamond ameyasema hayo leo Februari 26,2025 wakati akiingia kwenye tuzo za muziki za Trace zinazofanyika Zanzibar Kisiwani Unguja.

“Imagine Arusha kunatengenezwa uwanja mwingine. Tungepata Arena na sisi ingetusaidia, hizi event zikifanyika nyingi zinatukuza. Wasanii wa Kitanzania tumejitahidi sana kuweka nguvu ya kisanaa ambayo inaonekana.

"Kwa hiyo tunaomba serikali ituunge mkono kwenye kutuwekea Arena. Na itasaidia vitu vingi, Basketball, Netball, kutafanyika mikutano na mambo mbalimbali. Sanaa ya Tanzania ni kubwa sana lakini kwa sababu tunakosa vitu kama Arena unakuta watu wanaenda kwenye nchi za watu wengine,” amesema Diamond

Aidha nyota huyo wa muziki ameongezea kwa kutolea mfano nchini Rwanda wanavyonufaika na Arena zao

"Mimi msanii naongea na Basata kila siku lakini sitaki kuamini kama fedha hamna ni kuamua tu naamini Dkt Samia Suluhu Hassan ni mtu ambaye ameleta mageuzi, katika vitengo tofauti tofauti tunamuomba na sisi kama wasanii atutengenezee Arena,” amesema Diamond

Hata hivyo msanii huyo amesema sababu ya kuchelewa kwa tamasha hili la utolewaji tuzo ni kutokuwa na mazingira rafiki.

“Umeona hii event yao imechelewa kuanza ni kwa sababu stage ilikuwa inadondoka. Yaani pale mazingira sio wezeshi, kungenyesha mvua hapa tungeaibika. Kwa hiyo tusaidieni,” amesema Diamond






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags