Derulo na Diamond kutumbuiza Komasava kwa mara ya kwanza

Derulo na Diamond kutumbuiza Komasava kwa mara ya kwanza

Mwanamuziki kutoka Marekani Jason Derulo anatarajia kutumbuiza remix ya ngoma ya ‘Komasava’ na Diamond kwa mara ya kwanza jijini Johannesburg.

Kupitia ukurasa wa Instagram wa Derulo ameweka wazi kuwa ikiwa leo Septemba 21 anasheherekea siku yake ya kuzaliwa basi ataungana na msanii mwenzake Diamond kutumbuiza ‘Komasava’ kwa mara ya kwanza.

“Afrika Kusini ni siku yangu ya kuzaliwa!! Ninakuja Johannesburg kwenye jukwaa la ‘DStv Delicious Festival’ Jumamosi hii, tarehe 21 Septemba!! Pia nitatumbuiza wimbo wa ‘Komsava’ pamoja na @diamondplatnumz kwa mara ya kwanza kabisa! Ah, jamani, tumejawa na furaha.

Tunatazamia sana kuwa hapo pamoja nanyi nyote, na tunatumaini kuwa mtakuja kwa wingi ili tuweze kufurahia pamoja kwa sababu tunataka kufurahia! Nipo njiani.” Ameandika Derulo

Komasava Remix ambayo Diamond amewashirikisha wasanii kama Jason Derulo ft Khalil Harisson na Chley imeendelea kupata mafanikio makubwa duniani kote huku mpaka kufikia sasa imefikisha zaidi ya watazamaji milioni 19 katika mtandao wa YouTube ikiwa ni mwezi mmoja tu kupita tangu kuachiwa kwake.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags