Denzel Washington Hajali Kuhusu Tuzo

Denzel Washington Hajali Kuhusu Tuzo

Mwigizaji kutoka Marekani, Denzel Washington ameweka wazi kuwa hana wasiwasi wowote baada ya kukosa uteuzi katika tuzo za Oscar huku akidai kuwa anajivunia sana kazi zake kuliko tuzo.

Wakati alipokuwa kwenye mahojiano yake ya hivi karibuni Washington ameeleza kuwa anamuda mrefu kwenye tasnia hivyo hana pingamizi wala mtazamo tofauti kuhusiana na tuzo hizo za Academy.

“Nimekuwa kwenye tasnia kwa muda mrefu, na sitaki kupoteza muda wangu nikijali kuhusu tuzo, najivunia sana kazi yangu nikiwa kwenye set na hiyo ndio furaha yangu na sio tuzo au kuchaguliwa kuwania tuzo zozote,” amesema Washington huku akiangua kicheko.

Washington, ni mmoja wa waigizaji maarufu na wenye mafanikio makubwa Hollywood, amewahi kushinda tuzo mbili za Oscar kama mwigizaji bora kupitia filamu ya Training Day (2001) na Glory (1989).

Aidha maneno hayo ya kutoteuliwa kwenye tuzo hizo ni baada ya kukosa uteuzi kupitia filmu yake ya Gladiator II iliyoachiwa Novemba 2024.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags