DAWASA kuzima mitambo yakuzalisha maji Ijumaa

DAWASA kuzima mitambo yakuzalisha maji Ijumaa

Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira (DAWASA) imetoa taarifa ya kuzimwa kwa mtambo wa kuzalisha Maji, Ruvu chini ljumaa October 23,2022, kuanzia saa 12 asubuhi mpaka saa 2 usiku ili kuruhusu matengenezo ya Bomba Kuu maeneo ya Mlalakuwa na Mwenge.

Maeneo yatakayoathirika ni pamoja na Bagamoyo, Zinga, Kerege, Mapinga, Mabwepande, Bunju, Tegeta, Mbweni, Boko, Salasala, Goba, Mivumoni, Kawe, Lugalo, Makongo, Chuo Kikuu, Mwenge, Kijitonyama, Mikocheni, Msasani, Oysterbay, Masaaki, Mwananyamala, Kinondoni, Hospitali ya Taifa Muhimbili, Magomeni, Kigogo, Chang'ombe, Keko, Kurasini, Kigamboni, Airport, Kiwalani, Buguruni, Kigamboni, Vingunguti, Ilala na Katikati ya Mji.

Aidha wakazi wa maeneo hayo wameshauriwa kuhifadhi maji ya kutosha wakati wa matengenezo ili kuepukana na tatizo la kukosa maji kwa muda.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags