Dawa ya Mkongo yapigwa Stop

Dawa ya Mkongo yapigwa Stop

 

Hahahaha! Make hapa kwanza ncheke, wale vijana mliozoea kutumia mkongo mtaweka api sura zenu hahah! Nawasalimu kwa jina la mkongo

Mwenyekiti wa Baraza la Tiba asili na Tiba Mbadala Profesa Hamisi Malebo amesema Baraza hilo limeifungia dawa inayoitwa ya Hensha maarufu Mkongo yenye usajili namba TZ17TM0027.

Profesa Malebo amesema dawa hiyo ilikutwa imechanganywa na dawa ya kisasa ya nguvu za kiume inayoitwa Sildenafil kwa jina maarufu la biashara ni Viagra ama Erecto na kusema kuwa Baraza litaendelea kufungia wote wanaofanya kazi kinyume na Sheria.

"Baraza pia lilibaini dawa inayoitwa Hensha alimaarufu Mkongo yenye usajili namba TZ17TM0027 ambayo ilikutwa imechanganya na dawa ya kisasa ya nguvu za kiume inayoitwa Sildenafil kwa jina maarufu la biashara ni Viagra ama Erecto kitendo hiki ni kinyume na sheria na miongozo ya usajili wa dawa za tiba asili na mbadala”

“Baraza la Tiba Asili na Tiba Mbadala, kuanzia leo tarehe 27 Julai, 2022 limefuta usajili wa dawa ya Hensha alimaarufu Mkongo inayomilikiwa na kituo cha Nyasosi Traditional Clinic na ihakikishe dawa hiyo inaondolewa sokoni mara moja kuanzia leo vinginevyo hatua kali ya kisheria itachukuliwa dhidi ya Bw. Emmanuel Maduhu”

Pia, Prof. Malebo ameweka wazi kuwa, Kwa mganga ambaye anahitaji kutangaza dawa yake ni lazima afuate utaratibu wa kusajili dawa kwa kupima ubora na usalama na baadaye aombe kibali cha matangazo kutoka Baraza la Tiba Asili na Tiba Mbadala.

Aloooooweeeee! Haya una nini cha kusema au tukuache kidogo hahhha! unapata habari hii ukiwa wapi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags