Davis adai hana hatia, mauaji ya Tupac

Davis adai hana hatia, mauaji ya Tupac

Mshukiwa wa kwanza katika mauaji ya ‘rapa’ kutoka nchini Marekani #Tupac, #DavisKeefeD yalitokea mwaka 1996 amefikishwa mahakamani siku ya jana Alhamis ambapo kufuatia shauri hilo mshitakiwa huyo amekana na kudai kuwa hana hatia katika mauaji hayo.

#Davis alifikishwa Mahakama ya Wilaya ya Clark County, jana Novemba 2 ambapo baada ya mshukiwa huyo kudai tukokuwa na hatia katika mauaji ya Tupac, shauri hilo limepigwa kalenda hadi Novemba 7.

Davis Keefe D mwenye umri wa miaka 60 amekuwa kizuizini tangu akamatwe Septemba 29, mwaka huu wakati akiwa anafanya mazoezi karibu na nyumbani kwake Las Vegas.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags