Davido, Tems na Burna Boy kuwania tuzo za NAACP

Davido, Tems na Burna Boy kuwania tuzo za NAACP

Wanamuziki wanao ipeperusha Bendera ya #Nigeria #BurnaBoy, #Davido na mwanadada #Tems, wametajwa kuwania Tuzo za #NAACP kutoka nchini #Marekani.

Orodha ya wasanii na vipengele vya kuwania Tuzo hizo ilitolewa siku ya jana Alhamisi, Januari 25, ambapo Tuzo hizo zinatarajiwa kutolewa live Machi 16, mwaka huu kwenye channeli ya #BET.

#NAACP ni Taasisi ambayo imetoa Tuzo kwa zaidi ya miaka 50 huku lengo la kutoa Tuzo hizo kwa watu wote ni kupigania haki na usawa kwa watu weusi.

Aidha wasanii wengine wakubwa walioko katika kinyang’anyiro hicho ni pamoja na #ChrisBrown, #Drake, #Usher, Megan Thee Stallion na wengineo.
.
.
#mwananchiscoop
#burudikanasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags