Davido na Wizkid kutumbuiza jukwaa moja

Davido na Wizkid kutumbuiza jukwaa moja

Mashabiki wa muziki nchini Nigeria hatimaye watapata fursa ya kuwaona nyota wawili wanaopendwa zaidi nchini humo, Davido na Wizkid wakitumbuiza pamoja kwenye ziara ya pamoja ya muziki.

Siku ya Jumatano, Wizkid kupitia  ukurasa wake wa Instagram aliweka  tangazo lililowashangaza wafuasi wake wengi kuwa atafanya atatumbuiza jukwaani na nyota mwenzake Davido.

Katika ujumbe huo Wizkid aliandika, “Baada ya ziara yake ya ‘MLLE (More Love, Less Ego)’ !! Mimi na Davido tutafanya maonesho kwa pamoja! ili kuokoa pesa yako!

Inakumbukwa kuwa Wizkid aliripotiwa kuahirisha kutoa albamu yake ya 5 ya 'More Love, Less Ego' kufuatia kifo cha mtoto wa Davido, Ifeanyi.

Mashabiki walimsifu sana kwa kumuunga mwenzie mkono na kutoa heshima ya kipekee.

Wizkid na Davido waliwahi kutumia jukwaa moja mnamo mwaka 2017 mwezi Disemba katika tamasha la Wizkid ambapo Davido alikuja kama mgeni rasmi kutumbuiza.


Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post