Davido na Chioma watarajia kupata mtoto

Davido na Chioma watarajia kupata mtoto

Mkali wa Afro Pop, ambae anatamba na ngoma yake ya Unavailable Davido anatarajia kupata mtoto mwingine na mkewe, Chioma Avril Rowland.

Katika video waliyo post kupitia mtandao wa TikTok, inamuonesha Chioma akiwa amevalika gauni jeusi ambalo limeweka wazi ujauzito wake wakati alipokuwa jikoni anapika na mumewe Davido.

Wakiwa jikoni OBO alimrekodi video huku akimuita “Mke wangu, mpenzi, pete yako iko wapi?

Ikumbukwe tu wawili hao mwishoni mwa mwaka jana walimpoteza mtoto wao Ifeany Adeleke baada ya kuzama kwenye swimming pool lililoko nyumbani kwao.

 






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags