Davido atundika zaidi ya tsh 1.6 Bilioni shingoni

Davido atundika zaidi ya tsh 1.6 Bilioni shingoni

Kutokana na mafanikio aliyopata mwanamuziki Davido kupitia Album yake ya #Timeless, ameamua kujipongeza kwa kujizawadaia kidani cha thamani kilicho tengenezwa na madini ya Diamond inadaiwa gharama ya cheni hiyo inafikia Tsh  1.6 bilioni.

Tofauti na kujizawadia cheni hiyo, Davido ameonekana kufurahishwa na kazi zake zinavyozidi kukimbiza katika mitandao mbalimbali ya kuuzia muziki, kwani week iliyopita pia mkali huyo aliamua kujitunukia cheo kwa kudai kuwa yeye ndiye mwanaume wa mwaka.

Mkali huyo ndani ya mwaka huu amekuwa akizungumziwa sana katika mitandao mbalimbali ya kijamii  kutokana na kazi zake lakini pia jina lake lilizidi kutamkwa zaidi baada ya kudaiwa kuwapatia ujauzito wanawake wawili nje ya ndoa.

Vipi wewe umewahi kujizawadia kitu gani?






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags