David Beckham akaa foleni masaa 12 kumuaga Malkia Elizabeth II

David Beckham akaa foleni masaa 12 kumuaga Malkia Elizabeth II

Katika hali ya kustaajabisha na kufurahisha mwanasoka msaafu David Beckham weekend hii aliamua kukaa masaa 12 katika foleni ya kumuaga Malkia Elizabeth II, mjini London.

Badala ya kuruka mstari na kupewa "VIP treatement" kama mastar wengine, mchezaji huyo alikataa ofa ya kuruka mstari na kuamua kupanga mstari mrefu kama wananchi wengine wa kawaida.Akipokuwa akihojiwa na mtangazaji wakati yupo katika foleni hiyo ya kuelekea Westminster Hall, Beckham alisema kuwa 'hiyo ilikuwa ni experience ya kuipata na watu wengine.' 

"Tunataka kuwa pamoja, tunataka kusherehekea pamoja maisha ya Malkia wetu na nina hisi kitu kama hiki nikizuri kukihisi na wengine," aliongeza Beckham.


Aidha, mchezaji huyo aliyewahi kuzichezea timu za Machester United na Real Madrif alisema kuwa amekaa katika foleni hiyo kwa masaa 12 na magoti yake yako sawa ila mgongo ndio una maumivu. 

 

Baada ya kupata nafasi ya kufika katika ukumbi huo ambao Malkia Elizabeth II anaagwa, Beckham alionekana kuinamishwa kichwa na kulia kwa uchungu.Ikumbukwe kuwa enzi za uhai wa Malkia, Beckham alifanikiwa kupata bahati ya kukutana nae mara kadhaa na kupata bahati ya kuhudhuria hata harusi za kifalme.
Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Detricia Pamba

A Digital Journalist, Content Creation Executive at Mwananchi Communications Ltd and Chief Editor of Mwananchi Scoop. I'm also writes stories around Technology, every Wednesday on Mwananchi Scoop. My other famous segments on Mwananchi Scoop include LISTI and WHO’S HOT.


Latest Post