Daktari ashinda shindano la urembo ambalo walikatazwa kutumia make-up

Daktari ashinda shindano la urembo ambalo walikatazwa kutumia make-up

Mrembo Natasha Beresford mwenye umri wa miaka 26 ambaye pia ni mtaalam wa meno ameshinda shindano la urembo la Miss London 2023 ambalo washiriki hawakuruhusiwa kabisa kupaka kipodozi chochote usoni hata lip-bam.

Waandaji wamesema lengo la shindao hilo ni kuwaongezea wanawake kujiamini katika urembo asilia badala ya kuupa ‘promo’ urembo wa uongo uliojaa vipodozi.

Shindano hilo ambalo lilikuwa na washiriki 18 ambao wote walipigwa chini na mwanadada huyo ikiwa ni kwa mara ya kwanza katika historia ya miaka 95 ya shindano hilo.

Wakati washiriki wa shindano hilo miaka ya nyuma wakitakiwa kuwasilisha ‘picha’ zao bila, vipodozi wala ‘kueditiwa’ ikiwa ni sehemu ya shindano hilo, washiriki wa shindano la mwaka huu walipigwa marufuku hata kutumia mafuta ya midomo.

Baada ya kutwaa ‘taji’ la Miss London, sasa atashiriki ‘fainali’ ya Miss England, itakayofanyika mwaka huu.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags