D Voice aanza kuwavimbia wenzake

D Voice aanza kuwavimbia wenzake

Mwanamuziki wa Bongo Fleva nchini D Voice amedai kuwa yeye ndiyo msanii mdogo kutoka Afrika Mashariki anayerekodi video za mkwanja mrefu, huku akiwataka wanaobisha kuonesha mikataba ya malipo.

D Voice ameyasema hayo kupitia ukurasa wake wa Instagram na kummwagia sifa tajiri yake Diamond ambaye amekuwa akimlipia pesa za kurekodi video hizo.

“Kwa East Africa hii mimi ndiyo msanii mdogo ninaye-shoot video kwa hela nyingi kuliko yeyote anayebisha a-post mkataba wake wa malipo na mimi niposti, after all tajiri mawe anayo,” ameandika

Utakumbuka kuwa msanii huyo tangu aingie wenye lebo ya Wasafi ametoa video saba kati ya nyimbo zake ni ‘Zoba’, ‘Bam Bam’, ‘Lolo’, ‘Umenifunza’, ‘Mtamu’, ‘Mpeni taarifa’ na ‘Turudiane’.

D Voice alitambulishwa kwenye lebo ya Wasafi Novemba 17,2023 huku utambulisho wake ukiungana na albumu yake iitwayo ‘Swahili Kid’ iliyobeba ngoma 10.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags