Cr7 afunguka muda wake wa kustaafu ‘soka’

Cr7 afunguka muda wake wa kustaafu ‘soka’

Mchezaji nyota wa ‘klabu’ ya  #Al-Nassr, #CristianoRonaldo amesisitiza kuwa hafikirii kustaafu ‘soka’ na ataendelea kucheza siku za usoni. kauli hiyo ya CR7 ambaye kwa sasa ana umri wa miaka 38, ilikuja baada ya kufunga mabao mawili kwenye ushindi wa mabao 4-3 dhidi ya Al-Ahli.

Wakati akifanyiwa mahojiano na chombo cha habari baada ya ‘mechi’ dhidi ya Al-Ahli,  Cr7 alieleza kuwa anapenda ‘soka’ licha ya umri wake kwenda na ataendelea kufanya hivyo hadi miguu yake itakaposema inatosha, alienda mbali zaidi na kusema anajisikia vizuri sana anapo isaidia ‘timu’ yake kupata ushindi katika ‘mechi’

Kwa sasa nyota huyo anaendelea kukimbiza Saudi Arabia, amefikisha mabao tisa , ametoa ‘asisti’ sita katika ‘mechi’ sita alizocheza mpaka sasa kwenye ‘klabu’ ya Al-Nassr.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags