CMB Prezzo adondoka na kukakamaa akifanyiwa mahojiano

CMB Prezzo adondoka na kukakamaa akifanyiwa mahojiano

Mwanamuziki wa Kenya CMB Prezzo, amekutana na changamoto ya kiafya iliyopelekea adondoke na kukakamaa mwili wakati akifanyiwa mahojiano kwenye uzinduzi wa 'reality show' ya msanii mwenziye Bahati liitwalo ‘The Bahati’s Empire’.

Kutokana na video mbalimbali inayosambaa kwenye mitandao ya kijamii zinamuonesha Prezzo akiwa amepata changamoto hiyo ya kiafya wakati akiwa kwenye zulia jekundu akifanyiwa mahojiano na waandishi wa habari.

Hata hivyo video hiyo imeonesha walinzi pamoja na wageni wa kwenye hafla hiyo wakimsaidia mwanamuziki huyo kupata huduma ya kwanza.

Aidha mpaka kufikia sasa bado hakuna taarifa maalumu ya ugonjwa unaomsumbua hadi kupelekea kuanguka kwake. Wasimamizi wa Prezzo pamoja na waandaji wa tamasha hilo wameeleza kuwa watatuoa taarifa rasmi ya tukio hilo.

Ikumbukwe kuwa siku ya jana Juni 6, 2024 mwanamuziki Bahati Kenya alifanya uzinduzi wa ‘reality Show’ yake ambayo itakuwa 'reality show' ya kwanza kutoka kenya kurushwa kupitia mtandao wa Netflix.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags