Cleyton Msosa kijana  anayefanya sanaa ya uchekeshaji

Cleyton Msosa kijana anayefanya sanaa ya uchekeshaji

Siku zote juhudi, kupenda kitu unachokifanya, kujua kwanini unafanya hicho kitu, na wapi unatamani kufika basi nikwambie tu  kuwa hizo  ndiyo njia ambazo ukizitilia manani zitakusaidia  kufikia  malengo yako ya hapo mbeleni .

Leo ni Ijumaa ya kwanza ya mwezi October namleta kwako Cleyton Msosa, kijana chipukizi anayefanya sanaa ya Uchekeshaji wima maarufu (Stand Up Comedy).

Akizungumza na Mwananchi Scoop, Msosa ameeleza kuwa ili mtu awezekufanya sanaa hiyo anatakiwa awe na hadithi zinazovutia lakini pia anatakiwa awe mcheshi.

Aidha alisema kuwa vijana wengi nowdays wameamua kujikita kwenye sanaa hiyo kutokana na kuamini kuwa huenda ikabadilisha maisha yao ya hapo baadaye kama yeye anavyoamini hilo.

Vilevile amesema uchekeshaji wima unamanufaa makubwa sana kwake,  kwani moja ya manufaa aliyoyapata ni kufahamiana na watu wengi na kuweza kwenda sehemu mbalimbali.

Hata hivyo alieleza kuwa yeye yupo makini sana na kile ambacho anakifanya tofauti na vijana wengine wanavyoichukulia kazi hiyo, akiamini kuwa ndiyo njia na funguo ya kufungulia milango katika maisha yake.

Akizungumzia uhalisia wa sanaa hiyo alisema kuwa kwa sasa sanaa hiyo imekua tofauti sana  na hapo awali ilipokua inaanza.

“Kiukweli siwezi kusema naiona wapi sanaa ya uchekeshaji wima miaka ijayo lakini naangalia ilipotoka na sasa hivi jinsi tulivyopiga hatua tulivyoanza tulikua na comedy platform chache”alisema na kuongeza

“Ila hadi sasa hivi ziko nyingi sana kuna Cheka tu, kuna punchline, watubaki, uni comedy, street comedy watu wa Chuo cha maji wanafanya stand up comedy, zote comedy, na  special comedy sasa hivi imebadilika kuliko ilivyokua mwanzo tumepiga hatua kubwa sana” alisema .

Hata hivyo alisema ili kijana aweze kufikia malengo yake lazima azingatie mambo makuu matatu ikiwemo kuwa na juhudi, kupenda kitu unachofanya na wapi unataka kikupeleke ukifahamu hayo inakua rahisi kufaulu.

Vilevile aliweka bayana malengo yake katika siku za usoni akidaikuwa anatamani sana kuja kuiwakilisha Tanzania kimataifa na kuweka mipango kwa wasanii chipukizi wajao kwa kuwawekea njia bora, na kuhakikisha wazazi wanakuwa na mawazo chanya juu ya kazi za sanaa.

Nataka kuhakikisha wazazi waone kwamba sanaa  inaweza kubadilisha maisha ya mtu kama alivyofanya Mbwana Samatta kwenye mpira na Mwakinyo kwenye ngumi wamebadilisha mawazo ya wazazi na kuona sanaa pia ni maisha”

Sambamba  na hayo alizungumzia juu ya  uwelewa wa jamii kwa sasa  dhidi ya sanaa ya uchekeshaji wima na kubainisha kuwa jamii kwa sasa inatambua uwepo wa sanaa hiyo.

“kwa jamii inayonizunguka kwa asilimia 15 au 16 hivi wameanza kuwa na uelewa juu ya sanaa hii ni jambo la kumshukuru Mungu Coz mwanzo walikuwa hawaelewi wanasema nyie ndo mnafanya vituko? Alisema na kuongeza

“lakini sasa hivi wanazungumza vizuri kwasababu wameanza kuona kwenye televishion hata mitandao ya kijamii ninachoshukuru zaidi wazazi wangu  nao wametambua kazi ninayoifanya”alisema.

Kila jambo lina ugumu wake na changamoto zake Clyton alieleza ugumu anaokutana nao kwenye kazi hiyo.

“ Bado kuna maeneo mengi nchini hawajaelewa nini maana ya uchekeshaji wima, hiyo ni moja lakini nyingine wenyewe kwa wenyewe tunaibiana content kwani kufanya hivyo hatuwezi kukuza tasnia yetu”alisema.

Mafanikio anayojivunia

“Moja ya mafanikio ambayo najivunia ni mwaka huu nimefanikiwa kufanya  comedy special yaani ni kama album kwenye muziki ambapo niliweza  kuperform kwa dakika 97 na nilifanyia mwanza ilipewa jina la   The story of Edward”alisema na kuongeza

“Kwangu mimi kama mchekeshaji ni mafanikio makubwa sana kwani kwa hapa bongo watu amabo tumeweza kufanya hilo ni wartatu tu akiwemo Nalimi, Deogratius na mimi mwenyewe hivyo nimafanikio makubwa sana”alisema.

Hata hivyo alitoa ushauri wake kwa vijana ambao wako mbioni kufanya Sanaa ya Uchekeshaji wima akiwataka kutokukata tamaa kutanguliza malengo yao na wafanye vizuri kila wanapopata nafasi.

“Watapitia mengi ya kuwakatisha tama, watatukana sana, watakatiliwa, wataonekana hawajui, wataibiwa material yao lakini mimi nawashauri wasikate tama wahakikishe wanafanya vizuri kila wanapopata nafasi kila unapokwenda kuperfome fanya kwa uwezo wako wote hatakama kukiwa na watu watano”alisema.

Aidha aliwataka wachekeshaji wenzie kupambana na kuacha kutegemea serikali, wahakikishe wanafanya mambo makubwa na ifike mahala serikali iwategemee wao na sio wao kutegemea serikali.

Cleyton amezaliwa mkoani Arusha ndani ya hospitali ya Mount Meru  na kufanikiwa kupata elimu ya msingi na sekondari, na kujiunga na  elimu ya Advance katika shule ya Majengo, alithubutu kujiunga na Chuo cha Maji lakini ali drop out mwaka 2018.

 






Comments 4


  • Awesome Image

    The realiest man they are few in this๐ŸŒ

  • Awesome Image
    Suleiman Abbas

    Clayton is one of the best comedians in TANZANIA and even in AFRICA. simply because he talks about his life,childhood adulthood and career wise. NO MEMES,NO COPYING JOKES NO FAKE SHIT. THIS BROTHER IS REAL AND FUNNY.

  • Awesome Image
    Pusha880

    This is how we go ๐Ÿค ๐Ÿ”ฅ๐Ÿšฌ

  • Awesome Image

    Ni vizuri kijana kufuata ndoto zako

Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Saphinia Suleiman

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, career, skills development and technology.


Latest Post

Latest Tags