Claudette: Ugonjwa wa Celine Dion hauna dawa

Claudette: Ugonjwa wa Celine Dion hauna dawa

Dada wa mwanamuziki maarufu duniani Celine Dion, anaye fahamika kama Claudette Dion, kupitia mahojiano yake ya hivi karibuni amedai kuwa hakuna dawa yoyote itakayoweza kumfanya Celine kupona.

Kupitia mahojiano dada huyo aliyofanya na chombo cha habari cha Canadian Le Journal de Montréal amedai kuwa, hakuna tiba ya ugonjwa unaomsumbua mdogo wake, isipokuwa kujipa matumaini ndiyo kitu cha muhimu.

Katika mahojiano hayo amedai kuwa kwa sasa Celine hutumia sindano mahususi za kinga mwili na dawa za kutulia maumivu ya misuli.
Dada huyo anadai kuwa jambo muhimu zaidi kwa Celine Dion ni kupumzika, na kughairisha safari zake alizokuwa akitaka kuzifanya mwaka huu






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags