Cillian Murphy akubali kurudi kwenye Peaky Blinders

Cillian Murphy akubali kurudi kwenye Peaky Blinders

Baada ya mwigizaji kutoka Ireland, Cillian Murphy kukataa ofa kutoka kwa Margot Robbie ya kurudi kwenye filamu ‘Peaky Blinders’ akiigiza kama Tommy Shelby hatimaye imeripotiwa kuwa mwamba huyo ataonekana tena kwenye filamu hiyo.

Kwenye moja ya mahojiano yake Murphy aliweka wazi kuwa amefurahi kushirikiana na Steven Knight na Tom Harper kwenye toleo lijalo la filamu la ‘Peaky Blinders’.

Netflix pia imethibitisha uwepo wa Murphy kwenye filamu hiyo iliyotengenezwa kwa ushirikiano wa filamu ya BBC na kuongozwa na Steven Knight na Tom Harper.

Ingawa Netflix haijaachia trela rasmi lakini Knight hapo awali alidokeza kwamba filamu hiyo italenga zaidi kwenye vita ya pili ya dunia iliyopewa jina la ‘Peaky Blinders at war’.


Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post