Chuo chabatilisha shahada ya Diddy

Chuo chabatilisha shahada ya Diddy

Chuo Kikuu cha Howard kilichopo Washington, D.C siku ya jana Ijumaa Juni 7, 2024 kilitangaza kuwa bodi yake ya nidhamu imebatilisha shahada ya heshima aliyopewa mkali wa Hip hop kutoka Marekani Diddy Combs kufuatia video yake iliyosambaa mwezi uliopita ikimuonesha akimpiga aliyekuwa mpenzi wake Cassie hotelini.

Diddy alipata Shahada ya heshima kutoka Howard mwaka 2014 lakini chuo hicho kinaibatilisha baada ya kugundua tabia yake.

Kupitia tamko hilo lililotolewa na chuo hicho limeeleza kuwa hawakubaliani na ukiukwaji wa maadili hivyo basi Diddy hafai tena kuwa na heshima ya chuo hicho.

Hata hivyo wameweka wazi kuwa chuo kimefuta jina la Diddy kutoka katika hati zote zilizomuorodhesha kuwa miongoni mwa waliopokea shahada ya heshima ya Howard, pamoja na kufuta makubaliano ya ufadhili wa masomo waliwahi kuweka mwaka 2023.

Ikumbukwe kuwa video ya Diddy akimshambulia mpenzi wake wa zamani Cassie ilionekana kwa mara ya kwanza katika runinga ya CNN ambapo shambulio hilo lilitokea mwaka 2016 huko Los Angeles ambako Diddy alikuwa safarini na mpenzi wake huyo ambaye mahusiano yao yalivunjika mwaka 2016.

Aidha baada ya video hiyo kusambaa Diddy aliibuka Kupitia ukurasa wake wa mtandao wa Instagram na kuomba radhi kuhusiana na tukio hilo huku akidai kuwa hakuwa kwenye utimamu wa akili na yuko tayari kwenda kupatiwa msaada wa kisaikolojia ili kuwa mtu mwema.


Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post