Chrisean achora tattoo ya Ex wake usoni

Chrisean achora tattoo ya Ex wake usoni

‘Rapa’ kutoka nchini Marekani #ChriseanRock amechora usoni tattoo yenye sura ya ex wake na mzazi mwenziye #Blueface ambaye kwa sasa anatumikia kifungo gerezani, kama ishara ya kumkumbuka.

Mwanamuziki huyo ame-share video kupitia ukurasa wake wa #Instagram ikimuonesha akiwa amechora tattoo hiyo na kuweka ujumbe unaotaka Blueface aachiwe huru.

Hata hivyo siyo mara ya kwanza Chrisean kuchora tattoo ya mzazi mwenziye aliwahi kuchora shingoni na kuifuta baada ya kuwa na migogoro kwenye mahusiano yao kabla ya kuachana.

Blueface anatumikia kifungo cha zaidi ya miezi 6 jela Los Angeles kwa kosa la kukiuka masharti ya dhamana katika mashitaka yake ya kuhusika  kwenye tukio la upigaji wa risasi nchini humo katika mji wa Las Vegas mwaka 2022,  na kumshambulia ‘baunsa’ katika klabu ya Los Angeles mwaka 2021.
.
.
.
.#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags