Chris Brown na tetesi za kupata mtoto

Chris Brown na tetesi za kupata mtoto

Moja ya story nyingine huko kwenye mitandao ni ya msanii kutokea Marekani, Chris Brown huwenda anatarajia kupata mtoto wake wa tatu.

Hiyo ni baada ya EX Girlfriend wake mwanamitindo Diamond Brown kuonesha ujauzito wake na kuwa inadaiwa anaweza kujifungua siku za hivi karibuni na hiyo ni kwa mujibu wa tovuti ya RapUp.

Bado mwanamitindo huyo hajaweka wazi kama Chris Brown ndiye baba wa mtoto huyo, lakini alithibitisha kuwa ni mjamzito kwa kupost katika IG yake.

Hata hivyo mpaka sasa bado Chris Brown hajazungumza suala hilo mahali popote pale kama ni kweli ama si kweli na ikiwa ni kweli nyota huyo RnB atakuwa na jumla ya watoto watatu.

 






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm


Latest Post

Latest Tags