Chris Brown amuonya Tigo Fariah

Chris Brown amuonya Tigo Fariah

Mwanamuziki kutoka nchini Marekani, Chris Brown amemtolea povu msanii Tigo Fariah anayedaiwa kuiga swaga zake na kujinadi kufanana na staa huyo.

Tovuti mbalimbali zimeeleza kuwa, Chris Brow amempa onyo msanii huyo ambaye hivi sasa anakuja kwa kasi kwa kigezo cha kujifananisha naye akimtaka kuwa yeye na ajikubali badala ya kumuiga.

“Huwezi kuwa kama mimi ni bora kuwa wewe tu na uache kuendelea na mtindo huo kabla sijakuchukulia hatua nyingine,” amesema.

Aidha Tigo amekuwa akichapisha maudhui kupitia ukurasa wake wa Instagram ambapo ameonekana kuiga swaga na kuvalia kama Cris Brown ambaye ameoneshwa kukasirishwa na kitendo hicho.

Baada ya Chris Brown kutoa onyo hilo watu wengi mitandaoni walionekana kuwa upande wa nyota huyo huku wakimsaidia kumshambulia Tigo Fariah.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags