Chris Brown afikishwa mahakamani kwa kushindwa kulipa mkopo

Chris Brown afikishwa mahakamani kwa kushindwa kulipa mkopo

Mwanamuziki Chris Brown anakabiliwa na mashitaka ya kushindwa kulipa mkopo wa dola 2 milioni alizokopa kwenye ‘benki’ ya City National .

Katika mashitaka hayo ambayo yamefikishwa mahakamani na City National Bank, yanadai kuwa ‘benki’ hiyo ilimkopesha Chris pesa kwa ajili ya kununua migahawa miwili ya Popeyes Chicken.

Hata hivyo licha ya kushindwa kulipa deni hilo hata ununuzi wa migahawa hiyo pia haukufanikiwa.

Madai hayo yamepelekwa mahakamani kwani tangu mwaka 2018 ‘benki’ hiyo ilianza utaratibu wa kukusanya madeni ya mikopo kwa wadaiwa wake akiwemo Chris Brown na rapper The Dream bila mafanikio.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags