Chin Bees amtuhumu Rayvanny kaiba idea yake

Chin Bees amtuhumu Rayvanny kaiba idea yake

Mwanamuziki Chin Bees amemshutumu msanii mwenzake wa Bongo Fleva Rayvanny kuwa ameiba idea ya wimbo wa ‘Nesa Nesa’ wimbo ambao amemshirikisha Diaomnd na Khalil Harrison.

Kupitia ukurasa wa Instagram wa Rayvanny katika chapisho aliloweka la promo ya wimbo huo Chin amekomenti kwa kuandika kuwa idea ya wimbo huo ni ya kwake na kuwa Vanny Boy alimkataza asiitumie.

“Nesa Nesa ni idea yangu tuliofanya wote years back na umegoma nisiitoe bila wewe alafu leo unaachia wimbo umeitwa Nesa Nesa hizi ni dharau, daah we jamaa miyayusho sana aiseee mbona Nesa Nesa tena yaani unadharau sana,” amendika Chin Bees

Wimbo huo ambao umeachiwa rasmi leo Desemba 5, 2024 hadi sasa umetazamwa zaidi ya mara elfu moja katika mtandao wa YouTube.

Hii sio mara ya kwanza kwa Vanny Boy kulalamikiwa kuiba idea za wasanii wenzake utakumbuka miezi michache iliyopita msanii Badest alimshutumu Rayvanny kuiba idea ya wimbo wa Sensema aliyomshirikisha Konde Boy.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags