Chidimma Adetshina kushiriki Miss Universe Nigeria

Chidimma Adetshina kushiriki Miss Universe Nigeria

Chidimma Adetshina (23) ambaye aliamua kujiondoa kwenye mashindano ya Miss South Africa kutokana na kubaguliwa kwenye shindano, kwa madai ya kuwa ni raia wa Nigeria, na sasa mrembo huyo ameweka wazi kukubali mwaliko wa kushiriki Miss Universe Nigeria.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram alishare video akidai kuwa amepokea mwaliko wa kushiriki katika mashindano ya Miss Universe Nigeria na tayari ameshakubali mwaliko huo.

“Habari nyote Jina langu ni Chidimma Vanessa Onwe Adetshina. Siwezi kuanza video hii bila kutoa shukrani zangu kwa watu wote wa ajabu ambao wamenionyesha upendo na msaada mkubwa.

Nimepokea mwaliko kutoka kwa Silverbird Group ambao ni waandaaji wa shindano la Miss Universe Nigeria ili kushiriki katika Miss Universe Nigeria 2024, na nasema hili kwa furaha kubwa kwa sababu nimeamua kukubali mwaliko huu” amesema Chidimma

Utakumbuka kuwa Agosti 8, 2024 Chidimma alijiondoa kwenye shindano la Miss Afrika Kusini baada ya kubaguliwa na raia wa nchi hiyo kwa kudai kuwa mrembo huyo ni raia wa Nigeria hivyo hana vigezo vya kushiriki katika shindano hilo.

Katika kauli yake hiyo ya kujiondoa kwenye shindano hilo Chidimma Adetshina aliweka wazi kuwa amefanya hivyo kwa ajili ya usalama wake na familia yake.

Aidha minong’ono hiyo ilianza kufuatia na Chidimma kuwa na uraia wa nchi zote mbili ambapo inadaiwa kuwa mwanamitindo huyo alizaliwa Soweto nchini Afrika Kusini, baba yake akiwa Mnigeria na mama yake akiwa ni raia wa Afrika Kusini kwa hivyo Chidimma anauraia wa nchi zote mbili.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags