Cheni ya akili bandia inayoweza kukupa kampani wakati wowote

Cheni ya akili bandia inayoweza kukupa kampani wakati wowote

Mwanafunzi aliyeacha masomo katika Chuo kikuu cha Harvard aitwaye Avi Schiffmann kwa mara ya kwanza amevumbua kifaa cha akili bandia (AI) kiitwacho ‘Friend’ kwa lengo la kupunguza upweke kwa binadamu.

Kifaa hicho ambacho kinatarajiwa kuingia sokoni Januari 2025 kitagharimu dola 99 ikiwa ni sana na Sh 267,300 kinauwezo wa kusikia mazungumzo yako na mtu mwingine huku kikitoa maoni kupitia ujumbe wa maandishi utakao ingia katika simu yako ya mkononi.

Licha ya kutoa ushauri katika mambo ya kimsingi kifaa hicho pia kinauwezo wa kumshauri na kuunga mkono mavazi ya mtumiaji.

Kupitia kifaa hicho baadhi ya wadau wameingilia kati suala hilo wakidai kuwa kifaa hicho kinaweza kuleta athari kubwa kwa watu kwani binadamu wataacha kujiweka karibu na binadamu wenzao na kubase katika teknolojia ili kupata usaidizi wa mawazo na kihisia.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags