Che Malone apata ajali, Simba yawatoa hofu mashabiki

Che Malone apata ajali, Simba yawatoa hofu mashabiki

Mchezaji wa ‘klabu’ ya Simba SC, Che Fondon Malone ameripotiwa kupata ajali ya gari usiku wa kuamkia leo maeneo ya Shule ya Feza Mikocheni wakati akitokea Airport alipokwenda kupokea ndugu zake.

Kwa mujibu wa mashuhuda, mlinzi huyo raia wa Cameroon hajaumia maana alikuwa amekaa siti ya nyuma lakini dereva wake mbaye alikuwa kaka yake ndiyo ameonekana kuumia kwenye mkono lakini haraka alikimbizwa hospitali na kwa taarifa zilizopo ni kwamba anaendelea vizuri.

Mseamaji wa ‘klabu’ hiyo Ahmedi Ally amethibitisha kwa kusema  kuwa nyota huyo yupo salama na kesho atakuwepo mazoezini kujiandaa na mchezo ujao wa Ligi ya Mabingwa Afrika.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags