Charles Mfinanga, Nandy ni binti yangu

Charles Mfinanga, Nandy ni binti yangu

Duuuuuuh! yanii sio powa yaani hatari na nusu, katika mitandao ya kijamii kumekuwa na gumzo matata sana baada ya mzee mmoja kujitokeza na kueleza kuwa mwanadada aliefunga ndoa juzi kati na kuisimamisha TZ, Nandy kuwa ni damu yake.

Mzee Charles Mfinanga amefunguka hayo katika mahojiano na moja ya chombo mcha habari cha hapa Nchini na kueleza kuwa “mimi na mama yake Nandy hatukuwa na tatizo lolote isipokuwa dada yake alimuonea wivu wakati nipo na yule mama akaamua kumtorosha na kumpelekeka sehemu nisio ijua” amesema Charles Godfrey Mfinanga

Aidha mzee huyo aliendelea kwa kusema kuwa “Nachotaka kumwambia Nandy kwamba kama anatambua kuna Charles Mfinanga Zaidi ya mimi awe huru nampa Baraka zote lakini ajue tu ni damu yangu, akinitambua anitambue au akinikata na anikatae ila ni mtoto wangu kwasababu mama yake aliondoka na ujauzito” amesema Charles Mfinanga

Mmmmmmh! Swali la kujiuliza siku zote alikuwa wapi asizungumze hili? Haya wanangu wa Mwananchi Scoop dondosha komenti yako hapo chini unakipi cha kumshauri mama kija Nandy.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags