Chanzo cha siku ya wanawake duniani

Chanzo cha siku ya wanawake duniani

Kila ifikapo tarehe kama ya leo Machi 8, dunia inaadhimisha siku ya wanawake. Wapo baadhi ya watu ambao huitumia siku hii kuwapa zawadi ndugu zao wa kike, wapo wanaoituma kwa kufanya makongamano mbalimbali yenye mijadala chanya kwa ajili ya wanawake.

Kupitia jarida hili Mwananchi Scoop imekuangazia chanzo cha siku ya wanawake 

Siku ya wanawake duniani ilitokana na juhudi za wanawake nchini Marekani, ambao waliandamana mwaka 1909 jijini New York  wakidai haki zao mbalimbali kama vile,  kupunguziwa muda wa kufanya kazi, ujira kuongezwa  na kupatiwa haki ya kupiga kura.

Siku hii kwa mara ya kwanza ilisherehekewa mwaka 1911 nchini Austria, Denmark, Ujerumani na Switzerland. Si vyema kuzungumzia histoia ya siku hii bila kutaja jina la Clara Zetkin, ambaye mwaka 1910 alitoa wazo katika mkutano wa kimataifa wa wafanyakazi wanawake uliofanyika Copenhagen Denmark kuanzisha siku maalum kwa ajili ya wanawake. 

Mkutano huo ulikutanisha wanawake 100 kutoka mataifa 17. Mwaka 1975 siku ya wanawake ilikuwa rasmi  baada ya kupitishwa na Umoja wa Mataifa.

Siku hii huwa na maadhimisho ya kitofauti katika mataifa mbalimbali yakizingatia kaulimbiu rasmi ya mwaka husika ambayo inatumiwa duniani kote . 

Katika siku hii ya wanawake zipo nchi ambazo wameipa heshima na kuiweka kama siku ya mapumziko. Kati ya nchi hizo ni Urusi na  China ambayo wanawake hufanya kazi nusu siku.

Licha ya kuwa na makongamano yenye mijadala mizito, siku hii husherehekewa pia katika baadhi ya mataifa kwa kupeana maua kama vile wafanyavyo nchini Italy na Urusi.

Kama ilivyokuwa lengo la siku katika kuleta ukombozi kwa wanawake vilevile bado inatumika kuleta mfanikio kwa wanawake kwa kukutana na kuzungumza mambo yao kwa pamoja huku wakiangalia mafanikio ya kazi zao na changamoto zinazowakabili 

Katika upande wa burudani wapo baadhi ya wasanii wa kike ambao wamekuwa wakipambania vipaji vyao kila kukicha na kuhakikisha wanafika katika levo za juu kwenye sanaa ya muziki, filamu, vichekesho, mitindo.

Kati ya wasanii hao yupo Zuchu mwenye wafuasi (3.18M) kwenye mtandao wa YouTube, Nandy (1.3M), Shilole(1 45K), Maua Sama (39 4K), Lady Jaydee (162), Phina (2 76K), Angle Nyingu (439K), Lamata, Hamisa Mobetto.

International Women's Day






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags