Ilikuwa ni mwanzoni mwa miaka ya 2000, kipindi hicho nilikuwa napiga maji kwa kwenda mbele kabla sijaamua kuacha baada kupata misukosuko kadhaa...
Nakumbuka siku hiyo mimi na walevi wenzangu watatu tuliamua kwenda kunywa pale Maeda Bar, maeneo ya Mwenge, kipindi hicho ndio Bar hiyo ilikuwa imefunguliwa, na huyo mwenzetu aliyetushauri twende huko alitupa sifa za hapo Maeda kuwa kuna totos za kufa mtu, na alituhakikishia kuwa tunaweza kujitwalia kwa bei poa tu na kwenda kutuliza mzuka wa Bierrrr.
Tulifika pale majira ya saa moja usiku, na kutafuta meza moja iliyoko kwenye kona, tulipokaa tu huyo mwenzetu ambaye alionekana kuwa mwenyeji wa kiwanja hicho akaenda nje ya ile Bar na kuja na totoz tatu zilizoshiba maeneo ya makalioni, totoz zenyewe zilikuwa zimevaa viguo ambavyo vimeacha sehemu kubwa ya miili yao ikiwa wazi.
Zile totoz zilijumuika na sisi na jamaa kwa kupenda maujiko akatutambulisha kwa wale mabinti, akianza na mimi ambapo alinitambulisha kwa jina la Gustavo ninatokea nchini Ureno, na mwenzangu mwingine alimtambulisha kwa jina la Kwaku Kunto kutokea nchini Ghana na mwenzetu wa mwisho alimtambulisha kwa jina la Dumisani Tshepo kutokea nchini Afrika ya Kusini.
Aliwaambia wale machangu kuwa tumekuja nchini kwa mualiko wa wizara ya madini na nishati ili kuwasaidia kuandaa mikataba ya uchimbaji wa dhahabu hapa nchini na tumefikia pale Sheraton Hotel, wale mabinti kusikia kuwa tumefikia Sheraton macho yakawatoka kama mjusi aliyebanwa na mlango, maana walijua bahati imewadondokea. Si hivyo tu, ili kukoleza ujiko aliwaambia kuwa tutakaa kwa muda wa wiki mbili au mwezi kama kazi hiyo haitakamilika, pamoja na yote aliwaambia kuwa hatujui Kiswahili bali Kiingereza lakini pia aliwaambia kuwa mimi naongea Kireno zaidi na kingereza kidogo na yeye ni mkalimani wangu. Basi baada ya ule utambulisho tukawa tunapata moja moto moja baridi huku tukisindikiza na nyama choma na ndizi mzuzu.
Maongezi yetu yalikuwa yametawaliwa na lugha ya kiingereza cha kuombea maji na mimi nilikuwa naongea kiingereza huku nikichomekea maneno mawili matatu ya Kireno na kiitaliano ambayo mengi nilikuwa hata sijui maana yake na wakati mwingine nikitaja majina ya wachezaji wa kireno katikati ya maneno ya kiingereza na kwa kuwa pombe ndio zilikuwa zikiongea wakati huo, nilimudu kabisa kubeba ule uhalisia, huku jamaa yangu akijidai kuwatafsiria.
Kuna wakati nakumbuka nilimwambia Amigo, comistas abrigado tuto bene, quivichino,' na jamaa akawaambia kuwa eti nimesema nimewapenda wadada wa Kitanzania na ningefurahi kama ningepata binti wa kumuoa na kwenda naye nchini Ureno. Huyu changu mmoja ambaye alikaa jirani na mimi alianza kujipigia debe kuwa yeye yupo tayari na wala nisihofu.
Kuna wakati aliwambia kuwa natafuta apartiment ili niweze kuwa na nafasi ya kujimwaga kwani Hoteli tuliyofikia yaani Sheraton sijaipenda kwa sababu vyumba vyake vina nafasi finyu na mimi huwa ninakuwa na mikutano ya mara kwa mara na waziri na maafisa mbalimbali wa wizara hiyo. Wale machangu walionekana kuamini kabisa na hapo nikawa nafanyiwa masaji huku nikinyweshwa bia.
Mreno feki nilikuwa nimewekwa kati huku nikitomaswa tomaswa.
Tuliendelea kunywa, mpaka mida ya saa sita usiku, tukaitisha bili yetu ili tuondoke, bili ilipoletwa, nikazama mfuko wa nyuma ili kutoa wallet, nikakuta patupu, nikaanza kujisachi kila mahali huku nikiwa nimetaharuki, kote nikakuta patupu. Wale wenzangu walionekana kunishangaa. Walleti yangu ilikuwa imetoweka. Mwili ukanisisimka na nywele zikanisimama na pombe zote zilinitoka maana ni mimi niliyekuwa kinara wa kuagiza pombe huku jamaa zangu wakinimwagia maujiko kuwa mimi ndiye Bosi wao. Nilijkuta nikiropoka. Aisee hawa machangu wamenichapa wallet yangu, hapa haondoki mtu,' wale machangu kwanza walishikwa na butwaa kusikia naongea Kiswahili fasaha kabisa. Mmoja wao akamuuliza mwenyeji wetu aliyetuleta pale, we kaka si umetuambaia huyu ni Mreno na hajui Kiswahili mbona anaongea Kiswahili tena cha Kizaramo kabisa'
Hapa hakuna cha Mreno wala Mfilipino, nasema nataka wallet yangu la sivyo patachimbika hapa.' Nilipiga mkwala huku nikiwa nimesimama, yule jamaa aliyetuleta akawa ananikanyaga mguuni kwa kunikonyeza huku akiniambia kwa kiingereza kuwa nisiongee Kiswahili nitaharibu dili. 'Hapa hakuna dili wala nini ninachotaka ni wallet yangu hawa mabaradhuli wezi kabisa wanataka kuniibia mimi mtoto wa Mwananyamala!
Nasema leo patachimbika, leteni walett yangu haraka kabla sijageuka wa bluu' nilizidi kuchimba mkwala, lakini wale machangu walionekana kushikwa na butwaa, wasiamini masikio yao jinsi Mreno mimi ninavyochonga Kiswahili, tena fasaha kabisa.
Changu mmoja aliyekaa upande wa pili wa meza akataka kunyanyuka akidai anataka kwenda toilet, nilimrukia na kumkamata pedo yake kwa dizaini ya Kipolisi wenyewe wanaita Tanganyika jeki, unakwenda wapi, huondoki hapa mpaka mrudishe wallet yangu' wateja wengine waliokuwepo meza za jirani wakawa wanashangaa kuona eneo la meza yetu limekuwa uwanja wa vita.
Nilimvuta yule changu na kumkalisha kwenye kiti kisha nikamuagiza mmoja wa wenzangu kwa mkwala tu kuwa aende kwenye gari akaniletee Bastola yangu iliyoko kwenye droo ya gari. Ule mkwala ulisaidia maana aliitoa ile pochi ambayo aliificha kwenye sehemu zake za siri na kunipa akidai kuwa alikuwa ananitania tu, nilijikuta nikimlamba makofi ya chap chap, na kama sio wale jamaa zangu kunishika labda ningepata kesi ya kujeruhi. Meneja wa ile Bar alipoona tafrani akaja pale kutaka kujua kumetokea nini, lakini akakuta mchezo mzima umekwisha, nikaenda kaunta na kulipa bili yangu kisha tukaingia kwenye gari na kuondoka zetu, tukiwaacha wale machangu na baadhi ya wateja wa ile Bar wakiwa na mshangao.
Leave a Reply