Changamoto wanazokumbana nazo wapaka  rangi za kucha

Changamoto wanazokumbana nazo wapaka rangi za kucha

Hellow! Wafanya biashara wenzangu, its another Friday kwenye chimbo letu la  biashara tukitoa nondo zinazohusiana  na wajasiliamali wazee wenzangu wa kuchakarika.

Basi bhana leo nimekusogezea biashara moja matata sana ambayo vijana wengi hulalamika kuwa ni ngumu kwa upande wao ambayo ni utengenezaji na upakaji wa rangi kwenye kucha.
Kabla hatujafika mbali bwana wacha nisikuache hivi hivi nikueleze kuhusiana na mwenendo mzima kuhusu biashara hii ambapo unaweza kuianza ukiwa na mtaji mdogo tuu.NAMNA YA KUANZISHA BIASHARA HII

  • Mtu anayetaka kuanza biashara hii anatakiwa awe na nia ya dhati na kuipenda biashara hiyo.
  • Anatakiwa kujua eneo atakalofungua ofisi kwa ajiri ya biashara hiyo.
  • Anatakiwa kujua aina ya wateja wake ili aweze kuweka ubunifu au kukabiliana nao mfano gharama ya upakaji wa rangi kwenye kucha,rangi gani pendwa nk
  • Anatakiwa awe na lugha nzuri kwa wateja wake pia kujua kwa uchache elimu ya biashara.

 

MTAJI NA VIFAA VYA KUANZA BIASHARA HII

Mtaji wa kuanza biashara hii inategemea na mfanyabiashara mwenyewe namna atakavyoitengeneza ofisi  yake kwa mapambo anayoyapenda,lakini kwa mtu anayeanza biashara hii bila kuweka mambo mengi anaweza kuanza na mtaji wa sh 80,000/=  pamoja na vifaa vifuatavyo

  • Msasa wa miguu 1pc=1000/=
  • Nail cutter 1pc=5000/=
  • Gundi 2500/=
  • Kucha 1 dazen 7000/=
  • Remover 1litre 12,000/=
  • Sabuni 1 litre sh 3000/=
  • Mashine inaanzia sh 30000/= na kuendelea kulingana na uhitaji wako.
  • Ndi fail 1 sh 1000/=
  • Rangi za kucha 1 dazen 18,000/=
  • Taulo1 2000/= ila unaweza kuongeza kulingana na matakwa yako

 

Hivyo ndo vifaa vinavyotumika kuianza biashara ya utengenezaji na upakaji wa rangi kwenye kucha ambayo ni biashara inayokuwa kwa kasi sana kila kona ya  jiji la Dar es salaam. Kutokana na wadada wengi kuvutiwa na urembo huo.

NA HIZI NDIZO CHANGAMOTO WANAZOKUMBANA NAZO WAPANGA RANGI ZA KUCHA

Kama inavyofahamika kila biashara haikosi changamoto tena kwa biashara kama hii ambayo soko lake kuu ni wadada, Mwananchi Scoop ilizungumza na baadhi ya wafanyabiashara na kueleza changamoto wanazokutana nazo katika biashara hiyo.


  • Wateja kuwa wasumbufu wakati wa utengenezaji wa kucha

Mteja anapokuja kupaka rangi au kutengeneza kucha mimi mtengenezaji kulingana na aina yake ya vidole au kucha naelewa namna gani ya kutengeneza kucha katika shape tofauti tofauti

Kama shepu ya box,mdomo wa kuku pia aina ya rangi itakayompendeza kulingana na rangi yake lakini changamoto inakuja pale mteja anakuona unavyompaka rangi ukimaliza anasema rangi hajaipenda so unaifuta na kumpaka nyingine ambapo hasara inakuwa kwangu kwenye vifaa pia muda.

  • Wateja kuwa na mazoea,

maana wateja wengine wanachukulia kujuana kuharibu biashara ya mtu na kama inavyofahamika soko letu ni wanawake lazima umakarimu ili kesho arudi tena au kukuletea wateja wengine hii inakuwa changamoto kwani wengine wanakuwa hawalipii huduma kutokana na mazoea,heshima na uaminifu mliwekeana.

  • Ushindani kuwa mkubwa

Hii pia ni changamoto ambapo inatufanya tufanye kazi nnje ya maadili ya kazi yetu ili kuwavutia wateja kwa huduma nzuri mfano kuosha miguu au kuwamassage miguu sio kitu kizuri ila inatubidi tufanye hivyo kama mbinu ya kuvutia wateja na kufanya tuonekane wahuni watengenezaji wa kucha.

  • Mteja kutovaa nguo nzuri anapokuja kupata huduma

Hii sasa ndo changamoto kubwa sana tunazo kumbana nazo, kuna baadhi  ya wadada wakija kutengeneza  mfano mtu kuvaa skerti fupi hii inatusababishia matamanio kwasababu na sisi pia ni binadaamu tumeubwa kutamani. Tunawaomba sana dada zetu wanaokuja kutengeneza kucha wajaribu kuvaa nguo za ustaarabu kidogo maana nasisi tuko kazini

Hahahahahah! Make hapa kwanza ncheke, ama kweli siri ya mtungi aijuaye kata, wafanyabiashara hawa wanakutana na changamoto nyingi kutoka kwa wateja wao ila mtaani tunawalaumu wao bila kujali upande wa pili ambao ni wateja wao.

Kama kawaida Kazi yangu kukusogezea fursa za biashara kazi kwako  kufanya uamuzi. Cha msingi ni wewe kutoangalia hizo changamoto ndo maana kabla haujaanza kuchakarika unatakiwa uwe na subraa na uvumilivu katika kila unacho kifanya usiangalie kuhusu changamoto wala faida wala watu wanasema nini wewe jitoe katika jambo lako.

 






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post