Changamoto wanazo kumbana nazo wafanyakazi za vibarua

Changamoto wanazo kumbana nazo wafanyakazi za vibarua

Mambo vip!! Mtu wangu wanguvu ni weekend tena tunakutana hapa hapa Mwananchi ili tuweze kujuzana machache kuhusiana na maswala mazima ya kazi.

Leo katika segment ya kazi tumekusogezea kazi za vibarua zinavyo onekana katika jamii. jamani hapa tuelewane unaweza ukafanya kibarua halafu ukachukulia poa tu watu wengine au jamii kiujumla wanaionaje hiyo kazi yako.

Kwanza kazi za vibarua ni kazi sizizo rasmi kwa maana kwamba kazi ambazo hazidumu unafanya one time then inaisha halafu unatafuta kazi nyengine hizi wanazijua wale wananchi watabaka la kati

Tunaishi kwenye dunia ya utandawazi mara nyingi nyumbani hatuna kazi nyingi kila siku.

Watu wanalazimika kuajiri wasaidizi na kuishi nao kwasababu za kiulinzi na usalama naukiangalia sikuhizi apartments nyingi zina uhakika wa ulinzi na usalama na hivi vyote vinakuwa sehemu ya kodi.

Zile kazi za kufua kama huna mashine na kupiga pasi, kuosha gari nk wakati huo huo kuna vijana hawana hata pesa ya kula wanatafuta kazi kama kupanda maua, kupanda mchicha, mboga mboga, kufua, kupiga pasi, kuosha gari.

Mbali na kulipwa ujira mdogo, wafanyakazi hao hawakatwi kodi wala michango ya mafao ya mifuko ya jamii, licha ya kazi kama za viwandani kuongoza kwa hatari ya kuumia kazini, vibarua wengi wanalalamika kuwa hawana bima ya afya wala kuwasilishiwa makato ya mafao hifadhi ya jamii.

Mwananchi Scoop inapata fursa ya kuzungumza na mmoja ya mfanayakazi wa kibarua kutoka Kongowe Ally Salum maarufu kama mpemba yeye anazungumza kwa undani kabisa kuhusu vibarua.

Salumu anaeleza hakuna kazi ngumu na yashida naupatikanaji wake hakuna uwelekeo ni wa kushtukiza au kubahatisha tofauti na wale wanao fanyakazi walizo ajiriawa anasema

“Asikwambie mtu vibarua ni vigumu unaweza ukaamka asubuhi ukaenda kibaruani ukaambiwa kazi hakuna kwasababu nikazi ambayo haina mkataba hauagani na bosi kuwa mmeandikishana sehem mtu unakurupuka tu uvumapo upepo ndio huko huko”alisema Salumu

Anaeleza kazi ya  vibaruani ni kazi ya watu kama yeye ambao hawana ujuzi wa moja kwa moja na watu wenye hali za chini hivyo sio kazi yenye matarajio na matokeo mazuri katika jamii.

“Kwanza hata ukiiumia kazini hiyo ni juu yako tofauti na muajiri akiumia ofisi itamhudumia lakini kwa sisi tunatafuta miambili halafu hiyo hiyo ukiumia ujitibie ukiangalia mtu una familia inauhitaji mkubwa inapelekea watu kuwa hata wezi maana vya halali vina kuwa ghali” amesema Mpemba

Hivyo basi kwa yeye anasema kazi ya kibarua haimfikishi popote nikutafuta pesa yakula na wakati wengine inaweza ikawa mtihani pia hata kupata pesa hiyo ya kula.

Team yetu haikutaka kuishia kwakijana huyo, punde si punde ikakutana na Mama zuhura ambae kazi yake yeye ni kugonga kokoto ndio kibarua chake kikubwa japo wakati mwengine kazi ya kugonga kokoto ikipotea huwa anaingia mitaani katika majumba ya watu kwaajili ya kutafuta tenda kama za kufua, kusafisha nyumba na hata kubeba maji ya wajenzi.

Anaeleza ameanza kazi za kutafuta vibarua ilimradi aendeshe familia baada ya mume kufariki na kumuachia familia kubwa peke yake.

“Kwasisi wajane tusio kuwa na taaluma yoyote na tuna familia inatulazimu kufanya vibarua ilimradi mkono uwende kinywa lakini sio kazi nzuri kwa sababu sio ya kudumu”alisema mwanamama huyo

Wanasemaga heri ya nusu shari kuliko shari kamili msemo huu una maana kubwa ni bora kuwa hata na hicho kibarua kuliko kukosa kazi  kabisa japo inaumiza nandiomaana wanetu wa uswazi wanasema wanafanya kazi ili mradi mkono uwende kinywani.

Japokuna watu waliosoma wenye degree zao wapo mtaani lakini kutokana na ugumu wa ajira hawana budi kufanya vibarua ili mradi wapate kuendesha maisha yao ya kila siku, sisi team ya Mwananchi Scoop tunasemaje usizarau kazi ulionayo maana wapo wengine nje wanaitamani kazi hiyo hiyo unayo izarau wewe. Kula chuma hichooooo!!!

 

 






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post