Cassper Nyovest amkingia Tyla kifua

Cassper Nyovest amkingia Tyla kifua

Masoud Kofii


Mkali wa muziki kutokea Afrika Kusini Refiloe Maele 'Cassper Nyovest' ameonesha kutopendezwa na maamuzi yaliofanywa na kamati ya ugawaji wa tuzo za South Afrikcan Music Award ‘SAMA’, kwa kutomzingatia 'hitmaker' wa wimbo 'Water' Tyla.

"Hakuna kitu kama hicho Tyla ameshinda Grammy kupitia wimbo wa water, lakini hajapata tuzo ya SAMA kama recodi bora wa mwaka hapa nyumbani. Haha mnatuchezea,"ameeleza

Hata hivyo tuzo hiyo ya Record Bora ya Mwaka ambayo Nyovest alitamani ichukuliwe na Tyla imechukuliwa na Mthandeni SK na wimbo wa ‘Paris’ aliomshirikisha Lwah Ndlunkulu

Licha ya Cassper Nyovest kuonesha kumpigania Tyla wadau na mashabiki wameonesha kutokumuunga mkono, wengi wao walitoa mawazo tofauti na kile alichowaza Nyovest

"Tyla amekuwa msaliti kwetu na wala hayo mafanikio aliyopata Marekani hayana maana yoyote hapa Afrika Kusini. Wasikilizaji wa muziki wa Afrika Kusini ni tofauti na hao wa Marekani sisi tuna style zetu tunapenda kama amapiano, gospel na maskandi" Shabiki alimjibu Nyovest kupitia mtandao wa X

Water ya kwake tyla iliachiwa mwaka 2023 na kufanya mapinduzi makubwa kwenye muziki dunia hadi kubeba tuzo kubwa duniani kama Chaguo la Watazamaji 2024, tuzo za MTV, Tuzo za BATAZAI na tuzo za GRAMMY huku ikifanyiwa remix na rapa anayesumbua kwa sasa Travis Scott






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags