Cassie avunja ukimya, awashukuru mashabiki

Cassie avunja ukimya, awashukuru mashabiki

Baada ya kusambaa kwa video ya mwanamuziki na dansa Cassie akishambuliwa na aliyekuwa mpenzi wake Diddy, hatimaye Cassie amevunja ukimya na kutoa neno la shukrani kwa mashabiki, ndugu na watu wake wa karibu ambao wameonesha kuumizwa na video hiyo.

Cassie kupitia ukurasa wake wa Instagram ame-share ujumbe huo wa shukurani huku akiweka wazi kuwa pole anazozipata kwa mashabiki zimefanya nafsi yake itulie na ajisikie yupo salama licha ya tukio hilo kuvunja moyo wake lakini kwa sasa yupo sawa.



“Asante kwa kila mtu ambaye amechukua muda wake kulichukulia jambo hili kwa uzito ninachoomba ni kwamba kila mtu afungue moyo wake na kuwaamini waathiriwa wengine kwani ni ngumu sana mtu kusema ukweli uliyoyapitia.

“Natoa mkono wangu kwa wale ambao bado wanaishi kwa hofu usijikatie tamaa hakuna anayepaswa kubeba uzito huu peke yake, safari ya uponyaji haina mwisho lakini msaada huu unamaanisha kila kitu kwangu asante,” ameandika Cassie.

Ikumbukwe kuwa siku tano zilizopita runinga ya Cnn ilivujisha kwa mara ya kwanza video ya mkali wa hip-hop Diddy akimpiga Cassie kwenye hotel ambayo walikuwa pamoja iliyopo jijini Los Angeles nchini humo mwaka 2016.

Hata hivyo, baada ya video hiyo kusambaa Diddy alijitokeza kupitia ukurasa wake wa Instagram na kuomba radhi kufuatia na tukio hilo kwamba anaomba radhi kwa kile kilichotokea huku akidai kuwa hakuwa kwenye utimamu wa akili na yuko tayari kwenda kupatiwa msaada wa kisaikolojia ili kuwa mtu mwema.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags