Cardi B akabiliwa na kesi ya ukiukaji hakimiliki

Cardi B akabiliwa na kesi ya ukiukaji hakimiliki

Mwanamuziki wa Marekani Cardi B ameshitakiwa na wasanii wawili nchini humo kwa madai ya kutumia baadhi ya mistari yao katika wimbo wake wa ‘Enough’ bila kuwapa taarifa.

Kwa mujibu wa nyaraka za kesi iliyopatikana na TMZ News zimeeleza kuwa Kemika, na Sten Joddi, wamedai kuwa Cardi B na watayarishaji wake walitumia vipengele vya wimbo wao wa mwaka 2021 "Greasy Frybread" katika wimbo wa ‘Rapa’ huyo.

Imeripotiwa kuwa waimbaji hao kutoka mji wa Texas nchini humo wametoa mashitaka hayo dhidi ya Minaj mwenye umri wa miaka 31 mwezi huu na kudai fidia ya Dola 50 milioni.

Kesi hiyo pia inawataja Kikundi cha muziki cha Warner, na watayarishaji OG Parker na DJ SwanQo kama washitakiwa wenza waliyo sababisha wimbo huo utoke.

Utakumbuka kuwa Machi 15 mwaka huu ndiyo wimbo huo ulitolewa na uliingia kwenye orodha ya hits za 10 bora nchini humo.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi


Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post