Canada yabuni mbinu kupunguza matumizi ya Sigara

Canada yabuni mbinu kupunguza matumizi ya Sigara

Ikiwa tumezoea kuona maonyo mbalimbali kwenye chupa za pombe kama vile kunywa kistarabu, au yale ya kwenye sigara yasemayo uvutaji wa sigara ni hatari kwa afya yako, bila kutaja hatari hio ni zipi.

Sasa  Canada imekuwa nchi ya kwanza duniani kuchapisha onyo kali la moja kwa moja la kiafya kwenye kila karatasi ya sigara kwa kutaja madhara yatokanayo na uvutaji.

Hatua hii ni moja ya mikakati ya Wizara ya Afya Canada, kwenye kupunguza matumizi ya tumbaku na viwango vya uvutaji wa sigara ili kuokoa afya za raia wake.

Sigara hizo zenye ‘lebo’ ya onyo la kiafya kwenye sigara zimeanza kuonekana tarehe mosi mwezi huu kwenye baadhi ya maduka na inaelezwa kuwa hadi kufika mwaka 2024 maduka yote yanatakiwa kuwa na sigara hizo zenye ‘lebo’ ya onyo.

Maonyo hayo ya uvutaji sigara yamechapishwa kwa lugha ya Kingereza na Kifaransa yakiwa na jumbe mbalimbali kama vile “Sigara ni sumu kwenye kila pumzi”, “Sigara inasababisha saratani.” Uvutaji wa sigara ni hatari kwa watoto,”

Jumbe hizi kwenye karatasi ya sigara zinakuwa zinabadilika kwa kila sigara, lengo kuu ikiwa ni kupunguza matatizo ya kiafya yatokanayo na matumizi ya bidhaa hizo.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags