Camila atamani Drake na Kendrick Lamar wamalize ugomvi

Camila atamani Drake na Kendrick Lamar wamalize ugomvi

Mwanamuziki kutoka nchini Marekani, #CamilaCabello ametamani #Drake na #KendrickLamar wamalize bifu lao ambapo amedai kuwa watu wamekuwa wakimsema vibaya Drake.

Camila ameyasema hayo alipokuwa kwenye mahojiano na Gazeti la The Times, amedai kwamba inasikitisha kuona watu wakimsema vibaya Drake kwa sababu ya ugomvi wao na Lamar.

Hata hivyo katika mahojiano hayo amependekeza kuwa wanamuziki hao wamalize ugomvi ambayo unahusisha na masuala ya ushindani katika muziki.

.“Inasikitisha kuona watu wakisema mambo mabaya kuhusu rapper Drake ningependekeza siku wamalize ugomvi wao kwa sababu kila mmoja ni bora” amesema.

Utakumbuka Kendrick Lamar na Drake walianza kurushiana maneno baada J.Cole, Future na Metro Boomin kutoa wimbo wa ‘Like That’ ambapo Lamar alidai kwenye tasnia ya Hip-hop, yeye ndiye rapa mkubwa zaidi duniani na hana mpinzani.

Camila mwenye umri wa miaka 27 amewahi kufanya wimbo kama ‘Shameless’, ‘Senorita’, ‘My Oh My’, ‘Work Form Home’, ‘Better Place’ na nyingine nyingi.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags