Bwana harusi aua mama mkwe, Shemeji na Bibi harusi ukumbini

Bwana harusi aua mama mkwe, Shemeji na Bibi harusi ukumbini

Askari wa zamani na mwanariadha nchini Thailand, Chaturong Suksuk mwenye umri wa miaka 29 amewaua watu wanne kwa kuwapiga risasi akiwemo mke wake mwenye umri wa miaka 44 aliyefahamika kwa jina la Kanchana Pachunthuek, na kisha baadaye akajifyatua mwenye katika sherehe ya harusi yao waliofunga siku ya Jumamosi.

Inaelezwa kuwa tukio hilo lilitokea, baada ya Chaturong ambaye alikuwa bwana harusi siku hiyo kuondoka ghafla kwenye sherehe siku ya Jumamosi usiku na baadaye kurudi na bunduki na kisha kutekeleza tukio hilo.

Kati ya fariki kwa kupigwa risasi ni pamoja na mama mkwe wake, shemeji yake ambaye ni dada wa bibi harusi, na mgeni mualikwa mmoja.

Wageni wa harusi hiyo wameeleza kuwa walimuona bwana harusi akiwa hana furaha wakati wa sherehe. Kwa mujibu wa Polisi, wanaeleza kuwa bwana harusi alikuwa amelewa sana, japo sababu rasmi ya kufanya hivyo mpaka sasa bado haijajulikana.

Je wewe unahisi nini kilimkuta bwana harusi?
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags