Burna Boy kwenye orodha ya wanaovutia zaidi

Burna Boy kwenye orodha ya wanaovutia zaidi

Kwa mujibu wa jarida la Essence kutoka nchini Marekani limetoa listi ya mastaa wa kiume wanaovutia zaidi huku mkali wa Afrobeat Burna Boy akitajwa kwenye orodha hiyo.

Kwa mujibu wa Mhariri wa Essence, Rivea Ruff, ameeleza kuwa Burna ameingia kwenye orodha hiyo kutokana na mwili wake kuwa wa kuvutia zaidi, mitindo yake tofauti ya Kiafrika pamoja na sauti yake inayowavutia mashabiki akiwa jukwaani.

Orodha hiyo ya Essence ‘Sexiest Men Of The Moment’, inaongozwa na mwigizaji wa Uingereza Damson Idris, huku mastaa wengine walioingia katika listi hiyo akiwemo Usher, Colman, Trevente Rhodes, Daniel Kaluuya na Skepta.


Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post