Bruno aishangaza Man United

Bruno aishangaza Man United

Nahodha wa klabu ya Manchester United, Bruno Fernandes amewashangaza mabosi wa timu hiyo baada ya kuwa na mpango wa kuondoka katika kikosi hicho mwishoni mwa msimu huu

Kwa mujibu wa Sky Sport News imeeleza kuwa mchezaji huyo huenda akaiaga timu hiyo ambapo imedaiwa kuwa Bruno ameamua hatima yake hiyo baada ya kutamatika kwa mashindano ya Euro 2024.

Bruno ni mmoja wa wachezaji tegemeo katika kikosi cha Man United, akiisaidia klabu hiyo kutinga Fainali ya Kombe la FA mwaka huu ambapo watachuana na wapinzani wao wa jadi, Manchester City kwenye mchezo utakaochezwa katika uwanja wa Wembley, London.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags