BREAKING NEWS: Mzee Korongo afariki dunia

BREAKING NEWS: Mzee Korongo afariki dunia

Kwa taarifa zilizo tufikia hivi punde ni muigizaji mkongwe wa bongo movie Hamisi Korongo maarufu kama  Mzee Korongo amefariki leo katika hospitali ya mwananyamara jijini Dar es salaam.

taarifa za awali zinadai kuwa Mzee Korongo alilazwa hospitalini hapo akipatiwa matibabu siku chache kabla ya umauti kumkuta.

Taarifa hiyo imetolewa na moja ya msanii mashuhuri Susan Lewis maarufu kama Natasha Mamvi, kupitia ukurasa wake wa Instagram akiwa ameposti picha ya marehemu ilioambatana na ujumbe huu “  mzee Hamisi Korongo tulijitahidi lakini mungu amekupenda zaidi, pumzika kwa Amani” ameandika Natasha Mamvi

Msanii huyo mkongwe ambae alijipatia umaarufu kupitia baadhi ya movie na tamthilia ikiwemo siri ya giningi, mama kimbo na nyingine nying.

Taarifa Zaidi kuhusiana na chanzo cha kifo chake mwananchiscoop tutakujuza Zaidi.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags