BREAKING NEWS: Manara OUT miaka miwili

BREAKING NEWS: Manara OUT miaka miwili

Msemaji Mkuu wa klabu ya Young Africans (YANGA), Haji Manara amefungiwa kufanya shughuli za michezo nchini na nje ya nchi kwa miaka miwili, ikiambatana na faini ya shilingi milioni 20.

Kamati ya Maadili ya Shirikisho la soka Tanzania (TFF) imetoa maamuzi  hayo leo kuhusiana na sekretarieti kufungua kesi katika kamati hiyo dhidi ya afisa habari wa Yanga Haji Manara.

Kamati ya maadili ya TFF imemkuta na hatia Haji Manara kwa makosa ya kumvunjia heshima Rais wa TFF Wallace Karia.

Hatua hiyo imekuja baada ya Haji Manara kupishana kauli na  Rais wa Shirikisho la soka Tanzania (TFF) Wallace Karia katika eneo la VVIP wakati wa mchezo wa fainali ya Kombe la ASFC. kati ya Yanga dhidi ya Coastal Union.







Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Saphinia Suleiman

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, career, skills development and technology.


Latest Post

Latest Tags