Bodi ya ngumi Uingereza kuwanoa Watanzania wawili

Bodi ya ngumi Uingereza kuwanoa Watanzania wawili

Bondia wa zamani wa ngumi za kulipwa, Amos Mwamakula na aliyekuwa kocha wa mabondia wa kike nchini Comoro, Halina Abdallah Ally wamepewa fursa ya kujifunza namna ya kuwahudumia mabondia wanaopata majeraha 'cutting' wakiwa ulingoni.

Bondia na kocha huyo watajifunza nchini Uingereza kwa siku sita kuanzia Septemba 11-16 kozi ya cut man na corner man ambayo inawajengea uwezo wa namna ya kumhudumia bondia aliyepata majeraha au anayepaswa kuokolewa kwa kurushiwa taulo katikati ya mchezo..

Akizungumzia fursa hiyo, Mwamakula amesema inakwenda kuwajengea uwezo wa namna ya kuwahudumia mabondia waliopata majeraha katikati ya mchezo, namna ya kuwahudumia na kuwaandaa kiusalama kabla ya pambano.

Alisema, mbali na kuwahudumia majeraha, pia wataongezewa ujuzi wa namna bora na sahihi ya kum-second (kuwa msaidizi wa ulingo) kwa bondia katikati ya mchezo.

"Makocha wengi huwa wanafanya kiuzoefu, japo wachache wana utaalamu huo, na kwa hapa nchini Halima anakuwa kocha wa kwanza mwanamke kupatiwa mafunzo hayo," alisema Mwamakula.

Kozi hiyo imeandaliwa na Taasisi ya ngumi za kulipwa nchini Uingereza (APBC) na kusimamiwa na Kamisheni ya ngumi za kulipwa nchini humo (BIBA).

Akizungumzia ushiriki huo, Mwamakula ambaye ni mkurugenzi wa kampuni ya masumbwi ya Boxing kazi kazi alisema hiyo ni moja ya kozi ya ukocha wa ngumi yenye fursa kubwa.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post